Binti wa Eminem: Sina ujauzito

0
75

NEW YORK, Marekani

HAILIE Scott Mathers, ambaye ni mtoto wa kike wa staa wa muziki, Eminem, amewajibu mashabiki wake akiwaambia si kweli kwamba ana ujauzito.

Minong’ono ya ujauzito ilianza mara tu bibiye huyo mwenye umri wa miaka 25 aliposema ana hamu ya kupata mtoto.

Akikanusha hilo, Hailie anayetoka kimapenzi na mshikaji aitwaye Evan McClintock, amesema: “Bado, labda baada ya miaka miwili au mitatu.”

Katika hatua nyingine, amekiri kuwa baba yake, Eminem, naye ana hamu kweli kweli ya kuitwa babu.

Source: mtanzania.co.tz