Rick Ross ampongeza Mkangisa

0
71

NEW YORK, Marekani

RAPA mwenye jina na heshima kubwa kwenye soko la muziki duniani, Rick Ross, amempongeza staa wa filamu Afrika Kusini, Khanya Mkangisa, kwa kufikisha wafuasi milioni mbili kwenye mtandao wa Instagram.

“Hongera kwa kufikisha wafuasi milioni mbili. Sasa fanya wafikie milioni nne. Umenisikia?” ameandika Ross akielekeza ujumbe kwa Khanya mwenye umri wa miaka 33.

Khanya, ambaye pia ni mtangazaji wa vipindi vya televisheni, amejizolea umaarufu mkubwa, hasa kwa uwezo aliouonesha kwenye tamthilia ya Isidingo.

Kwa wafuatiliaji wa soka la muziki la Afrika Kusini, wanafahamu kuwa bibiye huyo anatoka kimapenzi na rapa J Molley.

Source: mtanzania.co.tz