Wanamitindo 20 kumnadia mavazi Ally Rehmtullah

0
78

NA MWANDISHI WETU

WANAMITINDO 20 wamechaguliwa kuonyesha mavazi ya wabunifu ambao wanahitimu katika masomo ya ubunifu yaliyokuwa yakiendeshwa kwenye shule ya Ally Rehmtulla.

Shoo hiyo ambayo imepewa jina la Dar Sunset Festival, itaambatana na ufunguzi wa ufukwe wa Coco Beach itafanyika Oktoba 16, 2021 itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serekali.

Majaji wakiwa katika usaili wa kupata wanamitindo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Rehmtulla amesema amechukua wanamitindo wanne wa kiume na 16 wa kike kwa ajili ya kuonyesha mavazi yake na wanafunzi wake.

“Tumepata wanamitindo 20 watanadi nguo nilizotengeneza na kubuniwa na wanafunzi wangu ambao tumewafundisha kwa muda wa miezi mitatu,”anasema Rehmtulla.

Vijana waliojitokeza katika usaili, kutafuta nafasi ya kunadi mavazi ya Ally Rehmtulla

Katika shoo hiyo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa hapa nchini pamoja na sanaa za asili.

Source: mtanzania.co.tz